Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #85

Hymn 85 Salama Tumepita

[V1]
Salama tumepita, safarini juma hii,
Tumwendee Mwokozi, atubariki sasa,
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma,
Siku hiyo ya raha, siku bora ya juma.

[V2]
Utupe nuru leo toka hazina yako,
Ondoa dhambi zetu, tupokee na pendo,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako,
Mikono yapumzika, tuishi ndani yako.

[V3]
Twakusanyika hapa, tusifu jina lako,
Ukaribie kwetu, tupe neema Bwana,
Utamu tusikize, wa raha ya milele,
Utamu tusikize, wa raha ya milele.

[V4]
Injili yako leo, ishike wenye dhambi,
Itupe nguvu nyingi, iponye wenye shida,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe,
Mioyo yetu shangaza, vyakula utulishe.

85. Salama Tumepita

Link copied to clipboard successfully!