Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #10

Hymn 10 Kristo wa Neema Yote

[V1]
Kristo wa neema yote, imbisha moyo wangu,
Mifulizo ya baraka, inaamsha shangwe kuu,
Unifunze nikupende, nikuandame kote,
Moyo wangu ukajae, furaha na tumai.

[V2]
Namshukuru sana Bwana, aniwezesha huku.
Salama aniongoza, hata kule nyumbani,
Yesu alinitafuta, njiani mbali kwake,
Akatoa damu yake, nipone hatarini.

[V3]
Kweli mimi mwiwa mkubwa, wa neema daima
Wema wako unifunge, zaidi kwako Bwana,
Ili nisivutwe tena, kukuacha ee Mponya,
Nitwalie moyo wangu, uwe wako kamili.

10. Kristo wa Neema Yote

Link copied to clipboard successfully!