Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #82

Hymn 82 Ni Siku ya Furaha

[V1]
Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru,
Nasi twaona raha, kuja kushukuru,
Leo watu wa Mungu, wadogo wakubwa,
Hukaribia mbingu, ilipo baraka.

[V2]
Leo ndiyo bandari, nasi twawasili,
Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili,
Kijito cha baridi, kimefanya ziwa,
Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.

[V3]
Leo ngazi na iwe, ifikayo juu,
Mawazo na yasiwe, ya duniani tu,
Leo ni kujilisha, chakula cha mbingu,
Na kujifurahisha, kwa mambo ya Mungu.

82. Ni Siku ya Furaha

Link copied to clipboard successfully!