Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #69

Hymn 69 Cha Kutumaini Sina

[V1]
Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana,
Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha.

[C]

Kwake Yesu, nasimama,
Ndiye mwamba, ni salama,
Ndiye mwamba, ni salama.

[V2]
Njia yangu iwe ndefu, yeye hunipa wokovu,
Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga.

[C]

Kwake Yesu, nasimama,
Ndiye mwamba, ni salama,
Ndiye mwamba, ni salama.

[V3]
Damu yake na sadaka, nategemea daima,
Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.

[C]

Kwake Yesu, nasimama,
Ndiye mwamba, ni salama,
Ndiye mwamba, ni salama.

[V4]
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani,
Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele zake.

[C]

Kwake Yesu, nasimama,
Ndiye mwamba, ni salama,
Ndiye mwamba, ni salama.

69. Cha Kutumaini Sina

Link copied to clipboard successfully!