Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #163

Hymn 163 Pengine Ni Saa

[V1]
Pengine ni saa ya kupambazuka, mishale ya jua
ipenyapo giza, kwamba atakuja Yesu mtukufu,
awapokee wake.

[C]

Bwana itakuwa lini, tutakapoimba,
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?”

[V2]
Pengine mchana pengine jioni, pengine usiku wa
manane, giza litatoweka kwa fahari akija, awapokee
wake.

[C]

Bwana itakuwa lini, tutakapoimba,
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?”

[V3]
Majeshi yake yataimba ‘hosana,’ na watakatifu
waliotukuzwa, watamsifu kwa kuwa amekuja,
awapokee wake.

[C]

Bwana itakuwa lini, tutakapoimba,
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?”

[V4]
Furaha tukiitwa pasipo kufa, pasipo kuona maradhi
machozi, kuchukuliwa winguni kwa fahari,
akija kwa watu wake.

[C]

Bwana itakuwa lini, tutakapoimba,
“Anakuja, Bwana Yesu, Aleluya, Amin,
Aleluya, Amin?”

163. Pengine Ni Saa

Link copied to clipboard successfully!