Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #157

Hymn 157 Mfalme yu Mlangoni

[V1]
Mfalme yu mlangoni, ndiye aliyetufia,
Mara wote wampendao, atawakusanya.

[C]

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama,
Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.

[V2]
Dalili za kuja kwake, zinazidi kutimizwa,
Karibuni wateule, watamlaki Bwana.

[C]

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama,
Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.

[V3]
Sitafute duniani, amani wala furaha,
Mpaka Bwana arudi, dhambi kuondoa.

[C]

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama,
Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.

[V4]
Tutakaa na Mwokozi, makaoni ya milele,
Daima tutafurahi, kuwa watu wake.

[C]

Yuaja, yuaja, mlangoni anasimama,
Anakuja, anakuja, kuja kwake karibu.

157. Mfalme yu Mlangoni

Link copied to clipboard successfully!