Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #158

Hymn 158 U mwendo Gani Nyumbani?

[V1]
U mwendo gani nyumbani? Mlinzi akanijibu,
“Usiku sasa waisha, macheo karibu,”
Usihuzunike tena, bali ulemee mwendo,
Hata ushike ufalme, kule mwangani juu.

[V2]
Na tena niliuliza, nchi yote ikajibu,
“Sasa mwendo watimika, milele karibu,”
Usihuzunike tena, ishara kuu zasonga,
Na viumbe vyangojea, sauti ya Bwana.

[V3]
Nikamwuliza shujaa, ndivyo kanitia moyo,
“Shikilia mapigano, kitambo yaisha,”
Usihuzunike tena, kazi ifanywe kwa moyo;
Tumeahidiwa tunu tuishapo shinda.

[V4]
Siyo mbali na nyumbani, fikara tamu njiani,
yatupoza roho nayo, yafuta machozi,
Usihuzunike tena, kitambo tutakutana,
Wenye furaha kamili, nyumbani mwa Baba.

158. U mwendo Gani Nyumbani?

Link copied to clipboard successfully!