Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #132

Hymn 132 Bwana ni Mchunga

[V1]
Majani mabichi malisho yangu.
Ananinywesha maji matulivu,
Atanirudisha nikipotea.

[V2]
Nipitapo bondeni mwa mauti,
U mlinzi wangu sitaogopa,
Fimbo yako yatosha kunilinda,
Ukinifariji sina hasara.

[V3]
Kati ya mateso meza waandaa,
Na kikombe changu kinafurika,
Umenipaka kichwani mafuta,
Nitaulizaje zaidi kwako?

[V4]
Wema na fadhili zinifuate,
Siku zangu zote hata milele,
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana,
Katika ufalme wa pendo lake.

132. Bwana ni Mchunga

Link copied to clipboard successfully!