Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #131

Hymn 131 Namtegemea Mungu

[V1]
131a Kwa Mahitaji ya Kesho Lord for Tomorrow and Its Needs
1
Kwa mahitaji ya kesho, sina ombi,
Unilinde nisitende dhambi leo,
Nisiseme neno baya, Mkombozi,
Nisifikiri uovu, leo hivi.

2
Ningefanya kazi sawa, na kuomba,
Ningekuwa mtu mwema, kila saa,
Mapenzi yako nifanye, na kutii,
Nitoe mwili dhabibu, leo hivi.

3
Kama leo ningekufa, kwa ghafula,
Nitegemee ahadi, zako Bwana,
Kwa mahitaji ya kesho, sina ombi,
Uniongoze nishike, leo hivi.

[C]
131 - Namtegemea Mungu1
Namtegemea Mungu niwapo, humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda, Baba wa mbinguni anilinda.


Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini), baharini
Moyo wangu (moyo wangu) aulinda (aulinda),
Baba wa mbinguni anilinda.

2
La waridi alinawirisha, na huyo tai juu angani,
Nami kweli ananilinda, Baba wa mbinguni anilinda.

3
Tunduni mwa simba namwamini, kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni, Baba wa mbinguni anilinda.

4
Bondeni mwa giza na upweke, mchunga wangu yu anilinda,
Kwa upole aniongoza, Baba wa mbinguni anilinda.

131. Namtegemea Mungu

Link copied to clipboard successfully!