Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #80

Hymn 80 Tupe Moto wa Uhai

[V1]
Tupe moto wa uhai, uliowaka zamani,
Uliowaongoza juu, wazee watakatifu.

[V2]
Wapi roho iliyokaa, moyoni mwa Ibrahimu?
Kadhalika ndugu Paulo, aliwezeshwa na moto.

[V3]
Kwani neema haina, nguvu siku hizi sawa,
Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?

[V4]
Zamani za kale Bwana, kumbuka na kwa rehema,
Zihuishe roho zetu, kwa Roho Mtakatifu.

80. Tupe Moto wa Uhai

Link copied to clipboard successfully!