Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #79

Hymn 79 Nataka Imani Hii

[V1]
Ambayo haitetemi kitu chote wakati wa shida,
Wakati wa shida.

[V2]
Isiyonung’unikia, huzuni taabu;
Lakini katika saa ya matata humwamini Mungu,
Humwamini Mungu.

[V3]
Imani inayong’aa, katika tufani,
Isiyoogopa giza wala shida njaa na hatari,
Njaa na hatari.

[V4]
Haiogopi dunia, kudharau kwake,
Haiangushwi na hila, nayo dhambi na udanganyifu,
Na udanganyifu.

[V5]
Bwana nipe imani hii, hivi nitaweza
Kuonja hapa chini ulimwenguni kurithi furaha,
Kurithi furaha.

79. Nataka Imani Hii

Link copied to clipboard successfully!