Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #78

Hymn 78 Mpaka Lini Bwana

[V1]
Mpaka lini Bwana, utakaa mbali?
Kumetuchosha moyo, kukawia hivi,
Utatujia lini, ili tufurahi,
Katika ile nuru, kuja kutukufu?

[V2]
Mpaka lini Yesu, utaacha watu,
Uliowakomboa, wawe na mashaka?
Wachache waamini, kwamba utarudi,
Wachache wa tayari, Bwana kukulaki.

[V3]
Waamshe watu wako, tangaza ujumbe,
“Mwe watakatifu, Bwana yu karibu,”
Utatujia lini, ili tufurahi,
Katika ile nuru, kuja kutukufu?

78. Mpaka Lini Bwana

Link copied to clipboard successfully!