Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #37

Hymn 37 Pendo Lako Ee Mwokozi

[V1]
Pendo lako Ee Mwokozi, hushinda pendo zote,
Kaa nasi ndani yetu, furaha ya mbinguni,
Yesu u rehema tupu, safi na kusamehe,
Mfariji mwenye huzuni, yaondoe machozi.

[V2]
Roho yako ya upendo, tuma kwa kundi lako,
Hebu tuirithi raha, iliyoahidiwa,
Uondoe moyo mbaya, u mwanzo, tena mwisho,
Timiza imani yetu, ili tuwekwe huru.

[V3]
Yesu uje kwetu sasa, tupokee huruma,
Rudi kwetu tena kamwe, usituache pekee,
Tungekutukuza leo, pamoja na malaika,
Imba na kutoa sifa, ingia kwa ibada.

[V4]
Sasa Bwana kazi yako, imalize moyoni,
Takasa hekalu lako, wokovu kamilisha,
Safisha viumbe vyako, katika wakati huu,
Tupumzike toka dhambi, tuingie mbinguni.

37. Pendo Lako Ee Mwokozi

Link copied to clipboard successfully!