Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #38

Hymn 38 Nasifu Shani ya Mungu

[V1]
Nasifu shani ya Mungu, mweneza bahari,
Muumba pia wa mbingu, jua nyota mwezi,
Ni tukufu yako shani, mtengeza mambo,
Ya nyakati na zamani, yasiyo na mwisho.

[V2]
Kadiri ya nionayo, ya kusifu Mungu:
Nchi niikanyagayo, na hayo mawingu,
Hakuna hata unyasi, usiokukuza,
Na upepo wavumisha, au kutuliza.

[V3]
Nami kwa mkono wako, naongozwa sawa,
Ni pato nikusifupo, kukwomba ni dawa,
Umenizingira nyuma, na mbele baraka,
Maarifa ya ajabu, yanishinda mimi.

38. Nasifu Shani ya Mungu

Link copied to clipboard successfully!