Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #200

Hymn 200 Baba Yetu Aliye Mbinguni

[V1]
Baba yetu aliye mbinguni, amenifurahisha yakini,
Kuniambia mwake chuoni, ya kuwa nami Yesu pendoni.

[C]

Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda,
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

[V2]
Nimuachapo kutanga mbali, yeye yu vivyo hupenda kweli,
Hunirejeza kwake moyoni, kweli yu nami Yesu pendoni.

[C]

Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda,
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

[V3]
Anipenda, nami ninampenda, kwa wokovu alionitenda,
Akanifilia Msalabani, kwa kuwa nami Yesu pendoni.

[C]

Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda, anipenda,
Anipenda Mwokozi Yesu, anipenda mimi.

200. Baba Yetu Aliye Mbinguni

Link copied to clipboard successfully!