Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #175

Hymn 175 Nitaonana na Yesu

[V1]
Nitaonana na Yesu, uso kwa uso kweli,
Siku ile shangwe tele, nikimwona Mwokozi.

[C]

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni,
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

[V2]
Sasa siwezi kujua, jinsi alivyo hasa,
Bali atakapokuja, nitamwona halisi.

[C]

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni,
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

[V3]
Mbele yake yafukuzwa, machozi na huzuni,
Kipotovu kitanyoshwa, fumbo litafumbuka.

[C]

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni,
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

[V4]
Uso kwa uso hakika, palepale furaha,
Nitafurahi kabisa, nikimwona Mwokozi.

[C]

Tutaonana kwa macho, huko kwetu mbinguni,
Na kwa utukufu wake, nitamwona milele.

175. Nitaonana na Yesu

Link copied to clipboard successfully!