Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #155

Hymn 155 Njiani Huniongoza

[V1]
Njiani huniongoza, Yesu wangu Mwokozi,
Rehema hatapunguza, milele kiongozi,
Ina raha kwandamana, duniani daima,
Nijaposumbuka sana, yeye hutenda vyema.

[V2]
Njiani huniongoza, hupunguza matata,
Nikiugua hupoza, na njaa ninashiba,
Lichokapo guu langu, nguvu zikapungua,
Jiwe lilo mbele yangu, hunibubujikia.

[V3]
Njiani huiongoza, kwa pendo lililo kuu,
Mwisho atanituliza, kwake Baba yangu juu,
Nikivikwa kutokufa, nikae na Mwokozi,
Nitamsifu sana sifa, kweli ni kiongozi.

155. Njiani Huniongoza

Link copied to clipboard successfully!