Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #127

Hymn 127 Nionapo Amani Kama Shwari

[V1]
Nionapo amani kama shwari, au nionapo shida,
Kwa hali zote umenijulisha, ni salama rohoni mwangu.

[C]

Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

[V2]
Ingawa Shetani atanitesa, nitajipa moyo kwani,
Kristo ameona unyonge wangu, amekufa kwa roho yangu.

[C]

Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

[V3]
Dhambi zangu zote wala si nusu, huwekwa msalabani,
Wala sichukui laana yake, ni salama rohoni mwangu.

[C]

Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

[V4]
Ee Bwana himiza siku ya kuja, panda itakapolia,
Utakaposhuka sitaogopa, ni salama rohoni mwangu.

[C]

Salama rohoni, ni salama rohoni mwangu.

127. Nionapo Amani Kama Shwari

Link copied to clipboard successfully!