Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #107

Hymn 107 Sauti ni yake Bwana

[V1]
Sauti ni yake Bwana, “Kwenda nani tayari?
Mavuno yanakawia, nani atayavuna?
Kwa kudumu anaita, zawadi atatoa,
Nani atakayejibu, “Nipo Bwana nitume.”

[V2]
Kama huwezi safari, hata nchi za mbali,
Pana watu karibuni, wasiomjua Yesu,
Kama huwezi kusema, jinsi ya malaika,
Waweza kuutangaza, upendo wa Mwokozi.

[V3]
Ingawa huwezi kuwa, mkesha mlangoni,
Ukiwatolea watu, nafasi ya uzima,
Kwa sala na kwa sadaka, watoa msaada,
Kama Haruni mwaminifu, kuinua mikono.

[V4]
Roho za watu zikifa, Bwana akikuita,
Usiseme kwa uvivu, “Hakuna kazi kwangu.”
Kwa furaha anza kazi, ile aliyokupa,
Ukajibu mara moja, “Nipo Bwana, nitume.”

107. Sauti ni yake Bwana

Link copied to clipboard successfully!