Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #62

Hymn 62 Napenda Kitabu Chake

[V1]
Napenda kitabu chake, kilichotoka mbinguni,
Barua kwangu ya Bwana, ujumbe wake wa pendo.

[V2]
Humo ndani ya kitabu, sura ya Yesu naona,
Karatasi zimekuwa, nyayo zake za kiongozi.

[V3]
Neno lake tamu sana, kama asali naona,
Natamani kulionja, ni mkate wa uzima.

[V4]
Mapenzi yake mwumbaji, yanafunuliwa humo,
Hazina kuu ya hekima, utajiri wa ajabu.

[V5]
Mwangaza wa ulimwengu, angaza humo moyoni,
Uwe mwandamizi pote, taa ya hatua zangu.

62. Napenda Kitabu Chake

Link copied to clipboard successfully!