Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #46

Hymn 46 Miguuni Pake Yesu

[V1]
Miguuni pake Yesu, maneno yake tamu,
Pahali palipo heri, niwepo kila siku.
Miguuni pake Yesu nakumbuka upendo
Na hisani yake kwangu, vimenivuta moyo.

[V2]
Miguuni pake Yesu, hapa mahali bora,
Pa kuweka dhambi zangu, mahali pa pumziko.
Miguuni pake Yesu, hapa nafanya sala,
Kwake napewa uwezo, faraja na neema.

[V3]
Unibariki Mwokozi, ni miguuni pako,
Unitazame kwa upendo, nione uso wako.
Nipe Bwana nia yake, ili ionekane,
Nimekaa na Mwokozi, aliye haki yangu.

46. Miguuni Pake Yesu

Link copied to clipboard successfully!