Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #27

Hymn 27 Tena Mwokozi Twalitukuza

[V1]
Jina lako lenye kupendeza,
Twangojea neno la amani,
Kabla hatujakwenda nyumbani.

[V2]
Tupe amani njiani mwetu,
Wewe u mwanzo u mwisho wetu,
Dhambini kamwe isiingie,
Midomo ikutajayo wewe.

[V3]
Utupe amani usiku huu,
Ili gizani kuwe nuru kuu,
Tulinde kwa kuwa kwako Bwana,
Usiku ni sawa na mchana.

[V4]
Tupe amani ulimwenguni,
Ndiyo dawa yetu majonzini,
Na ikitwita sauti yako,
Tupe amani milele kwako.

27. Tena Mwokozi Twalitukuza

Link copied to clipboard successfully!