Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #24

Hymn 24 Jina Lake Yesu Tamu Tukilisikia

[V1]
Jina lake Yesu tamu, tukilisikia,
Hutupoza tena hamu, hutuondolea.

[V2]
Roho iliyoumia, kwalo hutibika,
Chakula njaani pia, raha tukichoka.

[V3]
Jina hili ni msingi, ngao, ngome, mwamba,
Kwa hili napata vingi, kwangu ni akiba.

[V4]
Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani,
Mwanzo, Mwisho, na Amina, mali yangu yote!

[V5]
Moyo wangu hauwezi, kukusifu kweli,
Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.

24. Jina Lake Yesu Tamu Tukilisikia

Link copied to clipboard successfully!