Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #192

Hymn 192 Mwamba Wenye Imara

[V1]
Mwamba wenye imara, kwako nitajificha,
Maji hayo na damu, yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi, hunifanya mshindi.

[V2]
Kwa kazi zote pia, sitimizi sheria.
Nijapofanya bidii, nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa, ndiwe wa kuokoa.

[V3]
Sina cha mkononi, naja msalabani,
Nili tupu nivike, ni mnyonge nishike,
Nili mchafu naja, nioshe nisijafa.

[V4]
Nikungojapo chini, na kwenda kaburini,
Nipaapo mbinguni, na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe, rahani mwako wewe.

Text from Nyimbo Za Kristo · © respective copyright holders · shared for worship use

192. Mwamba Wenye Imara

Link copied to clipboard successfully!