Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #185

Hymn 185 Mungu U Mapenzi

[V1]
Mungu u mapenzi makamilifu, yapitayo fahamu za watu,
Twanyenyekea sisi wapungufu, wape baraka wapenzi wetu.

[V2]
Ewe Mapenzi yasiyopimika, twawaombea kitini Mwako,
Wape mapenzi yasiyotindika, waliooana mbele yako.

[V3]
Ewe uhai, wewe u dhamana, ya imani na matumaini,
Wape kuvumilia hapa sana wasiche maumivu mwishoni.

[V4]
Wape furaha hiyo iwezayo, kutia nuru kwenye huzuni,
Wape amani hiyo itokayo, katika matata duniani.

[V5]
Waende mbele kusaidiana, maisha yao ulimwenguni,
Hata mwisho, ni kuja kwake Yesu, wafurahi milele mbinguni.

185. Mungu U Mapenzi

Link copied to clipboard successfully!