Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #181

Hymn 181 Mahali pa Maji

[V1]
Mahali pa maji mazuri, maji ya uzima,
Anapotungojea Yesu, tutakaribishwa.

[C]

Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima,
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.

[V2]
Tunapochoka safarini, tamu kupumzika.
Panapo maji ya uzima, yatufurahisha.

[C]

Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima,
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.

[V3]
Una kiu? uje kwa Yesu, utaburudishwa,
Yesu yu maji ya uzima, unywe uokoke.

[C]

Mahali pa maji mazuri, penye maji ya uzima,
Tutakaa na Mwokozi, chemchemi ya uzima.

181. Mahali pa Maji

Link copied to clipboard successfully!