Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #137

Hymn 137 Saa Heri ya Sala

[V1]
Saa heri ya sala, tunapojidhili,
Kama tukija kwake Yesu rafiki,
Tukiwa na imani, kwamba yu mlinzi,
Waliochoka sana, watapata raha.

[C]

Saa ya sala, iliyo heri,
Waliochoka sana, watapata raha.

[V2]
Saa heri ya sala, ajapo Mwokozi,
Ili awasikie watoto wake,
Hutwambia tuweke, miguuni pake,
Mizigo yetu yote, tutapata raha.

[C]

Saa ya sala, iliyo heri,
Waliochoka sana, watapata raha.

[V3]
Saa heri ya sala, wawezapo kuja,
Kwa Bwana Yesu wanaojaribiwa,
Moyo wake mpole, atawarehemu,
Waliochoka sana, watapata raha.

[C]

Saa ya sala, iliyo heri,
Waliochoka sana, watapata raha.

[V4]
Saa heri ya sala, tutakapopewa
Mibaraka ya roho tukimwamini,
Kwa kuamini kweli, hatutaogopa,
Waliochoka sana, watapata raha.

[C]

Saa ya sala, iliyo heri,
Waliochoka sana, watapata raha.

137. Saa Heri ya Sala

Link copied to clipboard successfully!