Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #75

Hymn 75 Msingi Imara

[V1]
Msingi imara ninyi wa Bwana,
Umewekwa kwenu kwa neno lake,
Nini zaidi atasema Bwana,
Imani yenu ipate kuzidi?

[V2]
Wambiwapo vuka maji ya giza,
Mito ya mashaka haitazidi,
Takuwapo nawe nikuwezeshe,
Shida upatazo zisikutishe,

[V3]
Utakapopishwa ndani ya moto,
Nguvu nitakupa, upate pato,
Huteketezwi ila taka zako,
Na zitasalia dhahabu zako.

[V4]
Na mtu aliyenitegemea,
Nguvu za Jehanamu zijapotisha,
Kamwe kwa adui sitamtia,
Mtu wangu kamwe sitamuacha.

75. Msingi Imara

Link copied to clipboard successfully!