Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #60

Hymn 60 Pengine Siyo Mlimani

[V1]
Pengine siyo mlimani, utakaponiita,
Pengine siyo baharini, wala palipo vita,
Lakini unaponiita, na njia siijui,
Bwana nitajibu ni tayari, kwenda uniagizapo.

[C]

Ukiwa pamoja nami Bwana, mlimani baharini,
Niende utakaponiita; na fuata uendako.

[V2]
Pengine leo kuna neno, neno tamu la pendo,
Ambalo Yesu anataka, ninene kwa upole,
Ukiwa pamoja nami Bwana, nitamtafuta leo,
Yule aliyepotea mbali, nitasema upendavyo.

[C]

Ukiwa pamoja nami Bwana, mlimani baharini,
Niende utakaponiita; na fuata uendako.

[V3]
Pahali pako bila shaka, pa kuvuna shambani,
Kazi niwezayo kufanya, kwa Yesu Mkombozi,
Hivi nikikutegemea, kwa kuwa wanipenda,
Mapenzi yako nitayafanya, na niwe upendavyo.

[C]

Ukiwa pamoja nami Bwana, mlimani baharini,
Niende utakaponiita; na fuata uendako.

60. Pengine Siyo Mlimani

Link copied to clipboard successfully!