Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #54

Hymn 54 Nataka nimjue Yesu

[V1]
Nataka nimjue Yesu, na nizidi kumfahamu,
Nijue pendo lake tu, wokovu wake kamili.

[C]

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

[V2]
Nataka nione Yesu, na nizidi kusikia,
Anenapo kitabuni, kujidhihirisha kwangu.

[C]

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

[V3]
Nataka tena zaidi, daima kupambanua,
Mapenzi yake nifanye, yale yanayompendeza.

[C]

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

[V4]
Nataka nikae naye, kwa mazungumzo matamu,
Nizidi kuwaonyesha, wengine wokovu wake.

[C]

Zaidi zaidi, nimfahamu Yesu,
Nijue upendo wake, wokovu wake kamili.

54. Nataka nimjue Yesu

Link copied to clipboard successfully!