Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #49

Hymn 49 Ninaye Rafiki

[V1]
Ninaye rafiki naye, alinipenda mbele,
Kwa kamba za pendo lake, nimefungwa milele,
Aukaza moyo wangu, uache ugeuzi,
Ninakaa ndani yake, Yeye kwangu milele.

[V2]
Ninaye Rafiki ndiye, aliyenifilia,
Alimwaga damu yake, kwa watu wote pia,
Sina kitu mimi tena, nikiwa navyo tele,
Pia vyote ni amana, ndimi wake milele.

[V3]
Ninaye Rafiki naye, uwezo amepewa,
Atanilinda mwenyewe, juu ‘tachukuliwa,
Nikitazama mbinguni, hupata nguvu tele,
Sasa natumika chini, kisha juu milele.

[V4]
Ninaye Rafiki naye, yuna na moyo mwema,
Ni Mwalimu Kiongozi, mlinzi wa daima,
Ni nani wa kunitenga na mpenzi wa mbele?
Kwake nimetia nanga, ndimi wake milele

49. Ninaye Rafiki

Link copied to clipboard successfully!