Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #33

Hymn 33 Karibu Sana

[V1]
Karibu sana univute, karibu sana daima niwe,
Bwana napenda unishike, unilinde nisitengwe nawe,
Unilinde nisitengwe nawe.

[V2]
Karibu sana sina kitu, sina sadaka kwa Bwana Yesu,
Isipokuwa moyo wangu, uutakase katika damu,
Uutakase katika damu.

[V3]
Karibu sana wewe nami ninafurahi kuacha dhambi,
Anasa zote na kiburi, nipe niliyemsulibisha,
Nipe niliyemsulibisha.

[V4]
Karibu ssana hata mwisho, hata mbinguni nisimamapo,
Daima dawamu niwepo, nitakapoona uso wako,
Nitakapoona uso wako.

33. Karibu Sana

Link copied to clipboard successfully!