Back to Nyimbo Za Kristo List Nyimbo Za Kristo #30

Hymn 30 Yesu Unipendaye

[V1]
Yesu unipendaye, kwako nakimbilia,
Ni wewe utoshaye, mwovu akinijia.
Yafiche ubavuni, mwako maisha yangu,
Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.

[V2]
Ngome nyingine sina, nategemea kwako,
Usinitupe Bwana, nipe neema yako,
Ninakuamania, mwenye kuniwezesha,
Shari wanikingia, vitani wanitosha.

[V3]
Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako,
Niwapo mhitaji, utanijazi vyako,
Nao waangukao, wanyonge wape nguvu,
Poza wauguao, uongoze vipofu.

[V4]
Bwana umeniosha, moyo kwa damu yako,
Neema ya kutosha, yapatikana kwako,
Kwako Bwana naona, kisima cha uzima,
Mwangu moyoni Bwana, bubujika daima.

30. Yesu Unipendaye

Link copied to clipboard successfully!